Dongwe, Zanzibar Central/South Region, Tanzania
People interest: 0
07:00
3D
South Zanzibar
EASTER HOLIDAY TRIP; mwaka mpya 2022 umeshaingia na Easter imekaribia sanaa, vipi umeshajua wapi utakwenda kujivinjari katika siku Kuu ya Easter ? Kama bado basi sisi Jambo Trips Africa tumekuandalia bonge la trip kwenda Visiwani Zanzibar mwezi April kuanzia tarehe 16 hadi 18 Aprili,2022 yaani siku tatu za nguvu .Tunajua unahitaji kupata hewa mpya katika mazingira mapya na tulivu ili utulize moyo kujipanga vizuri kwa majumu ya mwaka 2022.
Kupitia Package hii ya Easter Holiday Trip, utapata fursa ya kutembelea vivutio maarufu vya kitalii huku tukihakikisha unapata malazi mwanana katika hotel ya kitalii ya nyota 3 kama tulivyokuorodheshea hapo chini ambazo utafurahia mandhari mazuri ya beach kali lakini pia vyakula vitamu vya Kizanzibari na Kitanzania bila kusahau ule urojo na pweza wa Zanzibar pale Forodhani wakati wa Sweet Evening break . Tumehakikisha kwamba wageni wetu wanapata wasaa wa kufanya utalii wa bahari kupitia Ocean Safari tour, lakini pia Utalii wa kihistoria kupitia Zanzibar STone town tour , na Utalii wa kitamaduni kupitia Zanzibar Spice Tour . Pia tunajua wewe una marafiki, ndugu au wazazi ambao ungependa kuwapelekea zawadi kutoka Zanzibar baada ya Easter Holiday trip na katika hili tumehakikisha wageni wetu wanapata wasaa wa kutembezwa katika maduka mbalimbali ya mjini Zanzibar ili wajinunulie kile wanachokitaka kwaajili ya wapendwa wao.
Karibu sana ujenge mazingira ya kupata mawazo mapya ya kimaendeleo kwasababu hii ni Trip ambayo inakupa wasaa wa kupata marafiki wapya wa ndani na wa kimataifa bila stress , si unajua tena jinsi ambavyo Dunia nzima hukutana Zanzibar katika visiwa vya kitalii !! Sasa unangoja nini ???
PACKAGE PRICE
EAST AFRICANS:
OUR RECOMMENDED HOTELS:
Hii inakupa vitu vifuatavyo
RECOMMENDED HOTELS IN EACH PACKAGE:
HAKIKISHA; umelipia Booking yako kabla ya tarehe tarehe 05 Aprili,2022 ili kuwa na uhakika wa nafasi yako katika Trip hii kwasababu tunafanyia booking zilizolipiwa tu na si vinginevyo. Katika orodha za hotel tulizoziorodhesha hapo Jambo Trips Africa itakuwa na uwezo wa kuongeza hoteli nyingine endapo moja itajaa .